Uchaguzi Tanzania

 
Tarehe 25 mwezi October ni siku maalumu kwa watanzania wote, kwani siku hiyo zoezi lilokuwa likisubiriwa kwa mda mrefu litatendeka.
Zoezi hilo la upigaji kura litasimamisha kazi mbalimbali za kijamii, ikiwa ni pamoja na ibada makanisani. Wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea waliojiandikisha ndio watapata fursa ya kuwapigia kura wagombea wanaowataka (kuanzia nafasi ya Udiwani, Ubunge na Uraisi) katika vituo vyao husika.
Zoezi hilo litakuwa la siku moja na kuanza saa moja asubuhi na kumalizika saa kumi jioni.
Kabla ya uchaguzi huo kufanyika kumekuwa na malumbano baina ya vyama, viongozi wa vyama na watu juu ya sheria kwa wananchi baada ya kupiga kura.
Wapo wanaosema inapaswa wapiga kura kuwa mita mia mbili mbali na kituo baada ya kupiga kura, kwani ndiyo utaratibu za uchaguzi wa Tanzania lakini wapo wanaosema utaratibu huu unapindishwa kwa kusema yapasa kurejea nyumbani baada ya kupiga kura.
Swali hilo limekuwa tata na wananchi wengi kubaki na maswali mengi juu ya mstakabali wa utaratibu unaopaswa kufuatwa baada ya kupiga kura.
Kikubwa ni kumuomba mwenyezi Mungu, uchaguzi ufanyike kwa amani na matokeo yakitoka yapokelewe kwa amani.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment