1. Utamkabidhi Msimamizi wa kituo kadi yako ya Kupigia Kura.
2. Nae atakihakiki kitambulisho chako na kulitaja jina lako kwa sauti kubwa ili mawakala wa vyama vya siasa waliopo kituoni wasikie.
3. Wasimamizi wa vituo na mawakala wa vyama vya siasa wakiwa na shaka na wewe, wanahaki ya kukuuliza maswali ili wajidhihirishe.
4. Msimamizi wa kituo atakukabidhi karatasi 3 za kura (Rais, Mbunge na Diwani) na pia atakuonyesha jinsi ya kukunja karatasi hizo.
5. Utaenda sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kupiga kura yako.
6. Utaweka alama ‘V’ ndani ya chumba kilichopo chini ya picha ya mtu mwenye umtakaye katika wazifa huo husika.
7. Utatumbukiza karatasi zako za kura katika masanduku ya kura kwa jinsi utakavyoelekezwa.
8. Kabla ya kuondoka, utachovya kidole chako kidogo cha mkono wa kushoto katika wino maalumu.
9. Ukimaliza zoezi hilo unaweza kukaa mita mia moja nje ya kituo husika cha kupigia kura.
0 comments:
Post a Comment