Mtikila alizaliwa mkoani Iringa nchini Tanzania, mwaka 1950. Amekuwa mwanasiasa tangu mwanzoni mwa miaka ya 90, pamoja na hayo alikuwa mwanaharakati wa haki wa binadamu kwa
kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho Liberty desk. Ukiachia mbali siasa na uwanaharakati aliokuwa akijishulisha nao, alikuwa Mchungaji mwanzilishi na mkuu wa kanisa la kipentekoste la Full Salvation Church. .Mwanzoni mwa miaka ya 90, mchungaji Mtikila alijipatia umaarufu mkubwa katika siasa za Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuongea, upinzani wake dhidi ya muundo wa muungano wa Tanzania,
Namo kabla kifo kumpata, tume ya uchaguzi haikumpitisha mwanaharakati huyo kuwania nafasi ya Uraisi kwa kushindwa kutimiza vyema baadhi ya masharti kama ile ya idadi ya wadhamini katika kila Mkoa.
Atakumbukwa kwa mengi, hususani uhodari wake wakuongea na kutetea kile alichoona ni sawa kutetea.
0 comments:
Post a Comment