Tangu kale katika kisomo changu nimekuwa nikielezwa
kuwa kuna uhuru wa mwanahabari, nikaelezwa pia juu ya uwepo wa taasisi
mbalimbali za kupigania haki za mwanahabari pamoja na binadamu ikiwemo taasisi
ya haki za binadamu.
Nilikuwa mwenye Imani kubwa na taaluma yangu,
nikiamini kuwa ni imara na yenye kuheshimika kama taaluma nyingine nchini na
duniani kote lakini leo hii nimetambua kuwa si hivyo bali ni maneno tuu.
Tazama leo hii, taaluma ya mwanahabari imepoteza
heshima yake na kufananishwa na taaluma ya waarifu ambayo imejaa uadui mkubwa
na polisi huku virungu vikiwa ni sehemu ya mawasiliano ya pande hizo mbili.
Kibaya zaidi ni pale ambapo taaluma hii huitwa taaluma ya uchochezi na vurugu.
Naam twatambua kuwa wanahabari wengi katika jamii yetu
ya Tanzania wamekuwa wakikutwa na mikasa kadha wa kadha wakiwa katika harakati
zao za kukusanya habari ndani na nje ya nchi yetu. Mikasa mingine ikilihusisha
jeshi la polisi na wengine kujeruhiwa pasipo julikana nani kamtendea hivyo.
Tazama hivi majuzi kabla ya marudio ya uchaguzi wa
Zanzibar, mwanadada kutoka idhaya ya kiswahili ya DW, Salama Saidi, alipotea
katika mazingira ya kutatanisha na hivyo kuzua maswali mengi kwa wanahabari
wetu juu ya uzima wake. Kitendo kilicho-lazimu jukwaa la habari kutoa tamko la
kulaani kitendo hicho pamoja na kuliomba jeshi la polisi kuingilia katika
kumtafuta mwanamama huyo.
Kwa uwakika kupitia hiyo mikasa, tunaona ni jinsi gani
maadhimio ya taasisi mbalimbali za kumlinda mwanahabari na taaluma yake
zinavyokiukwa lakini pia katiba ya sasa inavyopindishwa kwa kumyima mwanahabari
haki yake ya msingi ya kukusanya na kusambaza habari kwa jamii yake.
Sehemu ya 18 ya katiba ya Tanzania inabainisha kuwa kila mtu-
(a)
Anao
uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(b)
Anayo
haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi;
(c)
Anao
uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake,
na
(d)
Anayo
haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha
na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.
Hakika msomaji umejionea katiba ya nchi inavyosema
lakini mikasa kwa wanahabari haiishi kila kukicha.
Nina Imani ndugu msomaji unatambua juu ya mkasa wa
kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi ambaye alikuwa ni mwanahabari wa Channel
ten, ambapo kifo chake kilimkuta katika harakati za kutafuta habari lakini pia
tunakumbuka kitendo alichofanyiwa Saidi Kubenea cha kumwagiwa tindi kali
mwilini.
Si hayati Daudi Mwangosi na Saidi Kubenea waliokutwa
na mikasa hiyo pekee bali tunatambua kuwa kuna wenginie wengi waliokutwa na
mikasa tofauti tofauti ikiwemo ndugu yetu Jumbe Ismailly, Mwinyi Sadala,
Tegambwage na waandishi wengine wengi.
Ni dhahiri kuwa taaluma hii imepoteza uhai wake
kutokana na mikasa ambayo imekuwa ikiwakumba wanahabari kila kukicha, na hivyo
kupelekea wanahabari kukosa uwaminifu kwa serikali na vyombo vyake vya ulinzi
ambavyo vimekuwa vikisihii wanahabari waungane nao katika ujenzi wa jamii yetu.
Jambo ambalo limesababisha wanahabari wengi kusahau
nini taaluma yao inapawapasa kufanya kwa hofu ya kupata majeraha na kulinda
uhai wao kwani hata taaluma na sheria zilizotungwa nazo si kwa ajili ya
kumtetea mwanahabari bali zimepindishwa na kuwa msumeno mkali dhidi ya
wanahabari.
Swala la miiko ya habari, tuliyofundishwa pindi
tulipokuwa katika mafunzo ya uwandishi bora katika taaluma yetu ya uwanahabari
imekuwa ikitupiliwa mbali leo hii na kulazimu wanahabari walio wengi kusimama
na kutukuza yale serikali inafanya hata kama pale serikali inakosea na
inahitaji kukoselewa ili ijirkebishe.
Ni waandishi kadhaa leo hii wamekuwa tayari kuikosoa
serikali pindi ikoseapo huku wengi wakiwa wemejengwa kwa misingi ya kufuata
matakwa yao ya kiuchumi au ya wamiliki wao, wamiliki hao wengi wamekuwa
wakitulazimu wanahabari tuwe kasuku kwa kurudia yale washika dola wanayoyataka
kwa kuhofu na kulinda uhai wa chombo husika.
Hakika swali juu ya uhuru wa mwanahabari katika nchi
hii ni swali ambalo kila mwanahabari anapaswa kujiuliza na alitambue, japo ni
dhahiri kuwa uhuru wa taaluma hii ni wa wastani sana tangu kipindi cha mkoloni
hadi sasa.
Adhabu zilizopo juu ya mwanahabari ni kubwa kuliko ule
ulinzi aliopewa juu yake katika shughuli zake za kukusanya na kusambaza habari
juu ya jamii yake. Jambo linalomjaza hofu na kumlazimu kushindwa kufanya kazi
katika uwaridi mkubwa.
Imani yangu ipo juu ya Mheshimiwa Raisi Dokta John
Pombe Magufuli kupitia kauli aliyoitoa kuwa hatatuacha wanahabari kwani
atatuangalia na kutusaidia, japo sidhani kuwa jicho lake litajikita tuu katika
kufungia magazeti ila kuongeza uhuru wa habari na hili litawezekana kwa kutunga
sheria imara za kulinda wanahabari wote ndani ya nchi yetu Tanzania.
Lakini si kwa kutunga sheria na vifungu kandamizi
ambavyo vitamzuia mwanahabari ajikite katika katika ukweli bali akjikita katika
siasa ambayo imejazwa maigizo na utata mtupu. Itakuwa ni vyema vifungu hivyo
vimlinde mwanahabari katika nyanja zake zote za taaluma yake ikiwemo ukusanyaji
na usamabazaji.
Makala hii
imeandaliwa na mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Shule Kuu ya Uwandishi wa
Habari na Mawasiliano kwa Umma. Kwa mawasiliano zaidi
0 comments:
Post a Comment