HODGSON TUMBO JOTO


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza atatimuliwa endapo Uingereza itafanya vibaya kwenye mashindano ya UERO yanayoendelea nchini Ufaransa.

Kauli hiyo imetolewa na Chief wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza FA, Greg Dyke.

Amesema kuwa, endapo Uingereza itatinga nusu fainali za mashindano hayo Hodgson atalinda kibarua chake lakini ikiwa sivyo atatimuliwa mara moja.

Mkataba wa kocha huyu wa Three Lions utaisha mwishoni mwa mashindano haya ya UERO. Kocha huyo alianza kukifua kikosi hicho tangu mwaka 2012.

Uingereza wapo kundi B wakiwa vinara wa kundi lao wakiwa na pointi 4 wakiwafunga WALES kwa idadi ya mabao 2 kwa 1 katika mchezo uliopita wa kundi hilo linajumuisha timu za Slovakia na Russia.

Habari hii imeandaliwa na mwandishi wetu HASHIMU CHAMBUSO
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment