
Kwa kipindi kirefu Arsenal Wenger amekuwa akiwania saini ya Vardy kutoka Leicester City, kocha huyo aliamini kwa dau la paund mil 20 ingekuwa rahisi kumnasa mchezaji huyo.
Lakini bahati mbaya, harakati zake zimeshindwa kuzaa matunda kutokana na mkali huyo kudhamilia kubaki Leicester.
Mchezaji huyo sasa anaitumikia timu yake ya taifa ya Uingereza katika mashindano ya UERO yanayoendelea nchini Ufaransa.
Habari hii imeandaliwa na mwandishi wetu HASHIMU CHAMBUSO
0 comments:
Post a Comment