DUNGA ATIMULIWA BRAZIL



Kocha huyo ametimuliwa baada ya kushindwa kuiongoza Brazil vyema kwenye michuano ya Coopa America.
Pamoja na ushindi aliopata dhidi ya kikosi cha Haiti, shirikisho la nchi hiyo limeona lisitishe mkataba wa kocha huyo kwani ni fedhea kubwa kwa mabingwa mara tano wa kombe la dunia kufadhahishwa hivyo.
Ikumbukwe hii ni mara ya pili kwa Dunga kuwa mwalimu wa SELECA. Ambapo mwaka 2006 hadi mwaka 2010 alinoa kikosi hicho na kukipa kombe hili mwaka 2007. 
Mwaka 2010 Dunga alijivua ukocha baada ya kutoka hatua ya robo fainali ya kombe la dunia.
Dunga aliitwa tena kama kocha mkuu wa timu hiyo mwaka 2014 akichukua nafasi ya Luiz Felipe Scolari mpaka kufukuzwa kwake.
Habari hii imeandaliwa na mwandishi wetu HASHIMU CHAMBUSO, mwanafunzi wa shule kuu ya uwandishi wa habari na mawasiliano kwa umma.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment