Ni Muhammed Ali, wengi walimfahamu kama mkali wa ngumi, hasa kwa wale ambao walipata fursa ya kumuona akiwa ulingoni.
Aliweza kujizolea jina kubwa ndani na nje ya mipaka ya Marekani na wengi walitamani kuwa kama mkali huyo wa ngumi kwa ngumi zake nzito na kasi akiwa ulingoni.
Pamoja na kuwa mpiganaji hodari lakini pia alikuwa hodari kwa maneno, kwani aliweza kuwajaza jazba na hasira wapinzani wake kabla ya kuingia ulingoni na hivyo kuwaondoa mchezoni kabla ya pambano kuanza.
Hakika atakumbukwa kwa mengi, hususani kwa wale wapenzi wa masumbwi. Na wengi watamkumbuka kwa mapambano yake aliyoweza kucheza vyema na kutwa ubingwa wa mikanda kadhaa ambayo leo hii ni kumbukumbu kwa wengi.
0 comments:
Post a Comment