Mikasa ndani ya Uwanja wa Taifa katika mechi dhidi ya Nigeria

Huku mechi ikiendelea kati ya Taifa Starz na Nigeria (Super Eagles)matukio kadha yalijitokeza na kuwa kivutio na baadhi kuwa kero kwa watazamaji.
Kabla ya mechi hiyo kuanza, mashabiki walisikika wakimzomea Raisi wa TFF alipokuwa akikatiza pembezoni mwa uwanja na hivyo kumfanya kuelekea jukwaa kuu kwa upesi. Pamoja na tukio hilo, mashabiki walishuhudia kamera ambayo ni kama roboti ikipaa angani almarufu kama Camera drone ikifanyiwa majaribio katika uwanja huo kwa mara ya kwanza. Kabla ya mechi hiyo kuanza mashabiki walisikika wakiwazomea mashabiki wa timu ya Nigeria walipokuwa wakiwasili na hivyo kufanya polisi waingilia kati na kuwahamisha upande.
Image result for Mashabiki wa Taifa Stars katika mechi ya Nigeria
Waandishi wa habari nao walikutana na mzozo dhidi ya waandishi wa habari wa Azam baada ya waandishi hao kuwaomba waandishi wa mashirika mengine kuondoa kamera zao kwa kueleza kuwa mechi hiyo imeuzwa kwa Wafaransa. Tukio hilo lilikuwa gumu kiasi cha TFF na polisi kuingilia kati baada ya Wafaransa hao pamoja na TFF kushindwa kuwatoa waandishi wa habari wa makampuni mengine ya Tanzania.
Tukio jingine ni pamoja na Naibu Waziri kutoa amri ya kuruhusu mashabiki kuingia bure baada ya kuona mahudhurio hafifu. Nilipojaribu kujua sababu kuu ya mahudhurio hayo hafifu nilijuzwa kuwa ni kwasababu ya kiwango cha ada kuwa juu. Mashabiki hao walijibu amri hiyo kwa kuita jina la mgombea Raisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment