Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima amemkemea Dkt Slaa kwa yale aliyoyazungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya sababu zilizomfanya ajiondoa CHADEMA.
Alimuita muongo Dkt huyo kwani yeye ndiye aliyempeleka mh. Edward Lowassa mbele ya kamati kuu ya CHADEMA na kuiomba kamati hiyo imkubali kama mwanachama wake.
Kupitia ujumbe wa Dkt Slaa na mashahidi wawili aliombatana nao, alithibitisha kuwa Dkt huyo aliondoka katika chama hicho cha maendeleo kwa shinikizo la mke wake ambaye ndiye amekuwa kichwa cha familia na maamuzi.
Aliongeza kwa kumkemea Dkt huyo kwa kitendo cha kutumia usalama wataifa kama mgongo wa kuwatuhumu maaskofu na viongozi wakidini nchi kuwa walipokea fedha kutoka kwa Edward Lowassa kwa ajili ya kumuunga mkono katika harakati zake za kuwania Urais.
0 comments:
Post a Comment