Gbagbo alikuwa Rais wa Ivory Coast kabla ya kufikishwa katika mahakama ya kimataifa. Hii inatokana na yeye kukataa kutoka madarakani baada ya kushindwa Urais dhidi ya mpizani wake, jambo ambalo lilisababisha machafuko katika nchi hiyo na watu wengi kupoteza maisha kutokana na vita katikati yao.Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 na kupelekwa kizimbani mwaka huo huo.
Mapema Jumanne hii jopo la Majaji watatu lilizitupilia mbali hoja zote zilizotolewa na mwanasheria wa Gbagbo kuomba dhamana ya muda mfupi. Uamuzi huo uliotolewa awali unaoruhusu Gbagbo kuendelea kuwa kizuizini ulikuwa halali kwani iwapo ataachiwa kwa muda wowote lolote laweza kutokea kabla hukumu dhidi yake haijatolewa.
0 comments:
Post a Comment