Maandalizi ya ligi kuu bara yamezidi kushika kasi baada ya
timu nyingi zinazoshiriki ligi kuu msimu wa 2015/16 kusaini mikataba na makocha wa kigeni.
Usajiri huo wa makocha hao umekuwa kivutio kikubwa kwa
wapenzi wa soka na hata kwa mashabiki, kwani mashabiki hao wamejazwa na shauku
kubwa ya kuona nini makocha hao wataleta katika ligi kuu hii inayoanza tarehe
za usoni.
Baadhi ya makocha waliosajiliwa ni
kama Martin Glerics kutoka
(Uingereza) atakaefundisha Toto Africa,
Stewart Hall (Uingereza) atakaefundisha Azam, Hans Pluijm (Mholanzi)
atakaefundisha Yanga, Patrick Liewg (Mfaransa) atakaefundisha Stand United,
Dylan Kerr (Uingereza) atakaefundisha Simba na Mika Lonnstrom (Finland)
atakaefundisha Majimaji.Mashabiki wa timu husika wanaamini
uwepo wa makocha hao nchini utawapa changamoto makocha hao wazawa na hivyo
kuinua soka la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment