Unyanyasaji

Kwanini unyanyasaji wa wafanyakazi wa ndani ?
Tumezoea kusikia neno “unyanyasaji katika mazingira mbalimbali hasa katika maisha ya kila siku. Kila mtu akiwa na dhana yake. Wengine wakimaanisha kutokuwa na haki fulani katika kazi au nyumbani, vilevile wengine wakiwa na maana ya kutokupewa muda wa kutosha katika kazi ama shughuli fulani; na wengine wakiwa na maana kadha na kadha.
 Kwa ujumla hali ya unyayasaji ni hali ya kutokupata kwa muda haki za msingi. Wafanyakazi wa kazi za ndani, mara nyingi huchukuliwa kama wanawake/wasichana ambao wanafanya kazi mbalimbali za ndani, vilevile huchukuliwa kama wasaidizi wa kazi za ndani pamoja na watoto wadogo ambao wanakuwa wanahitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa wazazi wao mara nyingi kina mama. Wazazi wengi wa kike wanakua na kazi nyingi kiasi cha kushindwa kumudu kazi zingine za nyumbani. Hivyo hujikuta wakihitaji wasaidizi ambao hulazimika kuwalipa kwa namna moja au nyingine. Mara nyingine huenda na kumlea msichana wa kazi kwani wengi wao huwa ni wadogo kiumri ambao kwa mujibu wa sharia taratibu. Je hapo tuite ajira haramu wakati wanasaidia kazi za nyumbani? La hasha
Ni utaratibu ambao tumejijengea kuwalipa ujira kidogo pamoja na kuwapa mahitaji ya msingi haina maina ya kuwa ni mfanyakazi, kwani mfanyakazi lazima awe ameandika mkataba na muajiriwa, pia awe na umri usipungua miaka 18 na vilevile awe amejiunga na mojawapo ya vyama  vya wafanya kazi kama CWT, wafanyakazi serikalini au kwigeneko.
Hivyo kutokana na sababu ya kawaida wafanyakazi hawana sifa tajwa hapo juu. Hebu tuwaite wasaidizi wakazi za nyumbani. Mara nyingi hutafutwa ili kupunguza uzito wa kazi za nyumbani ikiwa ni pamoja na kazi za ndani, kuangalia bustani pamoja na uangalizi wa watoto nyumbani.
Hakuna asie kuwa na kazi za ndani ni nyingi, zinpoteza muda. Vilevile hakuna ubishi kwamba malezi ya mtoto yanahitaji umakini wa hali ya juu pamoja na kupoteza muda.
Hivyo hawa wafanyakazi wa ndani wanapaswa kulipwa kiasi kikubwa cha fedha, kupewa muda wa kufanya mambo yao ya kijamii ili wawe na tija katika kazi zao za ndani na nje.
Kinyume na matarajio haya; hawa ndio wamekua watu wa mwisho kabisa katika kulipwa kwani wengine wanalipwa kuanzia elfu ishirini na kuendelea kwa mwezi. Mfano mfanyakazi mmoja anaishi Tabata mawenzi, jina kapuni ameonesha namna ambavyo anaishi na familia yake mpya ya kazi, ambapo anafanya kazi saa kumi alfajiri, anafanya kazi bila kupumzika, vilevile anapewa chakula ambacho kimelala siku tatu.
 Binti huyu bado ni mtoto mdogo ambaye ana umri wa miaka kumi na tatu, kiasi kwamba hata elimu ya msingi hajamaliza. Ilipaswa awe darasa la sita ambapo hata kimakuzi bado hajamaliza makuzi kimofolojia kiasi kwamba anahitaji chakula bora pamoja na usingizi mzuri,ili akue vizuri.
Kama amekosa vitu hivyo,je unafikiri ataweza kufanya kazi katika ufanisi bora?Dhana ya unyanyasaji inajitokeza wazi pale mfanya kazi anapokosa ujira wake mzuri,ananyimwa muda wa kucheza pamoja na kushirikiana na watu wengine.Waajiri hawa wanafuata mawazo ya mwanafilosofia wa hoja ya kisayansi;Fredrick Taylor ambaye ana amini mfanya kazi lazima umuwekee sharia za kumbana ndio afanye kazi,kitu ambacho hakiwezekani,binadamu sio mashine,lazima mawazo ya mwanafilosofia mwingine wa hoja ya kiutawala,mfaransa Henry Fayol ambaye anasema kuwa mfanyakazi lazima apewe muda wa kutosha pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano.
Ukiachana na mfanyakazi huyo,yupo mwingine ambaye anaendelea kuthibitisha unyanyasaji wa wafanyakazi wa ndani.Huyu anatoka kimara baruti,ambapo ananyimwa muda wa kutosha pamoja na mshahara au ujira mdogo.Tofauti na aliyepita huyu [jina kapuni] ana miaka 22 hakupewa mshahara wake kwa mdaa wa miezi miwili,hivyo hakuona umuhimu wa kuendelea kufanya kazi bila kujaliwa.Kwa mfano hiyo dhahiri tunaona kwamba wafanyakazi wa ndani wanafanya kazi nzuri na ngumu,Bila hata chembe ya aibu na bado wanaangaliwa kwa jicho lisilokuwa na huruma.
Kutokana na hayo tunaona matatizo yanayojitokeza kutokana na unyanyasaji wa wafanyakazi wa ndani. Ndani nani je ya nchi. Tukianza na ndani ya nchi, mkoani Tanga, mfanyakazi mmoja wa ndani aljikuta akimalizia hasira zake kwa kumuwekea gundi kali “super glue” katika sehemu zake za siri, ambapo mtoto huyo mwenye miaka mitano, alikaa nayo kwa muda wa wiki mbili, na kuanza usikia maumivu ya tumbo na kibofu. Hili jambo ligundulika kupitia mtoto jinsi alivyokuwa anatembea.
Namalizia kwa kuangalia upande wa serikali, serikali hadi sasa hivi imeshindwa kuonesha makucha yake yake katika kukomesha vitendo hivi vya kikatili kwa wafanyakazi wa ndani. Wizara ya ajira na utumishi wa umma haina budi kufuatilia kwa ukaribu namna wafanyakazi wa ndani wanavyopatikana kwa kusaidiana na wizara ya jinsia na watoto. Kwani hii ni utumilikishwaji na ni ajira kwa watoto.
Makala hii imeandaliwa na mwandishi wetu Yokibeth Msuya.                                                                                          
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment