Siku 40 za wachimbaji waliofukiwa na kifusi
Wachimbaji waliofukiwa katika machimbo ya Nyangalata wilayani Kahama kwa siku 41 wameokoleewa wakiwa hai usiku wa kuamkia leo.
Watu hao wamedai kuwa walikuwa wakiishi kwa kula nguo zao, mende, chura, magome ya miti na udongo ardhini, huku wakitumia haja yao ndogo kama maji kwani hapakuwa na maji hata kidogo huko chini.
Waathirika hao wanadai kuwa kabla ya kula walikuwa wakiviombea vitu hivyo, jambo ambalo wanasema lilikuwa kinga yao dhidi ya magonjwa ya tumbo.
Hivi sasa waathirika hao wamelazwa katika hospitali ya Kahama.
Habari hii imeandaliwa na mwandishi wetu Rose James Kudema

0 comments:
Post a Comment