Barua ikisema
"Kuna
ujumbe umesambazwa kupitia mitandao ya kijamii ukieleza kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemthibitisha
Kaimu Mkurugenzi wa Mwasiliano ya Rais Ikulu Bw. Gerson Msigwa katika
cheo hicho na kwamba amemteua Bw. Jerry Murro kuwa Msaidizi wa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Ujumbe huo wenye kichwa cha habari kilichoandikwa "BREAKING NEWS" unasomeka hivi, nanukuu.
"Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amemthibitisha Ndg Geryson Msigwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu
huku msaidizi wake akiwa ni aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga Ndg
Jerry Muro" Mwisho wa kunukuu.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu inapenda kukanusha taarifa hiyo na kuwataka wananchi kuipuuza.
Ifahamike kuwa uteuzi wowote unaofanywa na
Mhe. Rais Magufuli hutangazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu
ama kupitia Mamlaka rasmi za serikali. Pia huwekwa katika tovuti rasmi
ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz
Kwa sasa Mhe. Rais John Pombe Magufuli
hajafanya uthibitisho wa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw.
Gerson Msigwa na wala hajamteua Bw. Jerry Cornel Murro kuwa Msaidizi wa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kama ilivyoenezwa. Pia hana
mpango wa kufanya uteuzi huo.
Ikulu inawaomba wananchi wote kuzipuuza
taarifa hizo na kuendelea na shughuli zenu za kila siku. Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Gerson Msigwa ataendelea
kuwapa taarifa kutoka Ikulu kupitia utaratibu rasmi ambao umekuwa
ukitumika."
Ikihitimishwa na
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
17 Julai, 2016
0 comments:
Post a Comment