Ndugu msomaji karibu ujumuike name katika makala yangu
inayojadili nafasi ya lugha ya Kiswahili na umuhimu wake katika matumizi hasa
vyuo vikuu.
Kwa kuanza ni shauku yangu kukujuza kwamba vyuo vikuu ni
miongoni mwa taasisi za juu za elimu ambapo watu hujiunga ili kusomea taaluma
Fulani kwa kina Zaidi. Mara nyingi taaluma hizo hutolewa katika kiwango cha
shahada, aidha stashahada nazo hutolewa. Mfano wa vyuo vikuu ni kama chuo kikuu Dodoma(UDOM),SAUT na UDSM.
Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha za kibantu, lugha
yenye historia ndefu yenye manufaa makubwa kwa Taifa la Tanzania. Chimbuko la
Kiswahili huelezwa kuwa ni upwa wa
Afrika Mashiriki na baadae kusambaa sehemu nyingi Duniani.
Tunapozungumzia uhuru wa Tanganyika, Tanzania ya sasa
itakuwa ni dhambi kubwa tusipokumbuka Kiswahili kwani kilikuwa kiungo muhimu
baina ya jamii za Tanganyika katika kupigania uhuru.
Itakumbukwa kwamba baada ya mkutano wa Berlin, bara la
Afrika liliangukia mikononi mwa wa koloni, na wakoloni waliotawala Tanganyika walilazimika
kujifunza Kiswahili ili kuweza kurahisisha shughuli zao, biashara za waarabu
ndiyo zilifungua uwanja mkubwa wa Kiswahili kwani kila kituo walichopita
waarabu kilikuwa kikubwa cha Kiswahili.
Matumizi ya lugha ya Kiswahili hasa katika taasisi za elimu
ya juu (yaani vyuo vikuu) yamekuwa yakiridhishwa na yanakumbwa na changamoto
lukuki ambazo zinahatarisha maendeleo ya Kiswahili.
Sioni ubaya wa kuruhusu matumizi ya Lugha ya kiswahili kama
lugha ya kufundishia katika taasisi ya elimu ya juu hususani vyuo vikuu, lugha
ni sehemu ya utamaduni hivyo kama hatutumi lugha ya kiswahili katika mazingira
ya wasomi tupo tayari kuu kana utamaduni wetu.
Kuna Imani miongoni mwa watu kuwa lugha ya kiingereza ndio
lugha inayofaa kutumika kufundishia vyuo vikuu, kuwapatia watu elimu na maarifa
ya kufanya kazi na ndiyo lugha ya biashara au ajira, kwangu mimi naona mtazamo
huu kama potofu, uliotawaliwa na ufinyu wa mawazo kwa yupo mwanasaikolojia
mmoja alisema “mtu akifundishwa kwa lugha yake ya asili kisukuma, ataelewa
Zaidi.” Na mahanisha lugha yetu ya kiswahili inajitosheleza kuwajuza watu elimu
kwa manufaa ya taifa.
Ingawa sera ya kufundishia vyuo vikuu ni lugha ya kiingereza
bado ni changamoto kubwa kwa walimu, sisemi kuwa hawajui kiingereza la hasha
bali ninachotaka kusema hapa ni kwamba baadhi yao ambao ni asilimia kubwa
hupenda kuchanganya lugha (code mixing) katika mihadhara yao wanaotoa. Sio kosa
lao kwani kazi ya mwalimu ni kumfanya mwanafunzi aelewa kwa namna yiseyote na
matumizi ya lugha zote mbili yaani kiswahili na kiingereza ni moja jitihada
hizo. Ni dhahiri shahiri kuwa lugha ya kiswahili ni lugha ya Taifa, kutokana
historia ya lugha hii kuwaleta watu pamoja ndiko kunakonifanya nijiuliza
kwanini kiswahili kitumike kwa kuibuiba wakati ni lugha rasmi ya Tanzania?
Aidha wataluma wa lugha hudai kwamba mtoto hujifunza na
kuielewa lugha kwa ufasaha zaidi, kuliko mtu mzima. Ni wazi kwamba mfumo wa
Tanzania wa elimu kuanzia elimu ya vidudu au chekechea hadi darasa la saba
ambapo kiingereza ni kama somo tuu, huku lugha ya kiswahili ikichukua nafasi
kubwa. Katika kipindi hicho mtoto ndio ana uwezo mkubwa wa kuifahamu lugha kwa
umakini, cha ajabu ni kuifanya kiyume pindi aingiapo kidato cha kwanza hadi
chuo kikuu, ambapo kiswahili hufundishwa kama somo na masomo mengine kutumia
kiingereza.
Maendeleo ya nchi yeyote ile huletwa na wataalamu wake
waliofundishwa kwa lugha za nchi zao na kuelewa na kubobea. Mfano ni nchi kama
China, Korea na Urusi ambazo zinamaendeleo ya juu kutokanana na kuzingatiia
matumizi ya lugha zao. Hivyo kama nasi tukiipa kipaumbele lugha yetu ya Taifa
basi na sisi kuna uwezekano mkubwa wa kupata kuendelea kichumi kama nchi taja
katika aya hii.
Wahenga walisema safari ni hatua na waswahili husema
tunajifunza kutokana na makosa. Sioni kama vibaya kwa Tanzania kuiga baadhi ya
sera nzuri zitakazo ifanya lugha ya kiswahili, lugha adhimu kuzidi kuwa na
mashiko katika nchi yetu. “sera ya matokeo makubwa sana” ilianza nchini Malaysia na imeleta mafanikio
makubwa na sasa naona ni wakati muafaka
kwa nchi ya Tanzania kukopa sera ya lugha kutoka nchi za magharibi
ilikuendeleza na kukuza lugha ya kiswahili. Kwani kwa kukopa huko kutachangia
katika ukuzaji wa uchumi na kupunguza matabaka ndani ya nchi.
Kwa kumalizia Makala haya, huenda wengine watakosoa matumizi
ya lugha ya kiswahili chuo kikuu.Kikubwa nachotaka kusema ni kuwa Kiswahili inajitosheleza
na inahadhi kulinganisha na soko la kimataifa. Pia lugha yoyote inayokuwa
lazima ikope msamiati mingine toka lugha zingine hivyo waandishi wa vitabu vya
somo lolote lile kwa manufaa ya Taifa letu na ili yote haya kufunikiwa lazima
sera ya elimu itazamwe upya na waandichi kuondoa kusumbaa na kuona lugha ya
kiswahili ni duni na kuzikweza lugha za mataifa mengine.
0 comments:
Post a Comment