Hatimaye Zidane avaa viatu vya Rafael Benitez


Kocha huyu  Rafael Benitez ametupiwa virago vyake nje ya uwanja wa Santiago Bernabe baada ya kushindwa kuifikisha timu ya Real Madrid katika ubora ulikuwa unategemewa na wakali hao.
Kitendo hicho cha kufukuzwa kwa kocha huyo kinakuja baada ya Real Madrid kutofanya vizuri katika ligi ya nyumbani hadi kushika nafasi ya tatu nyuma ya mahasimu wao Barcelona na majilani zao Atletico Madrid.
Pamoja na kuwa nyuma, matokeo ya Jumapili yalifedhehesha uongozi mzima wa Madrid baada ya kushuhudia suluhu dhidi ya Valencia na kuwa nyuma point 4 nyuma ya Atletico Madrid.

Uamuzi huo wa kumtimua Rafael unampa aliyekuwa kocha wa vijana katika timu ya Real Madrid Zinedine Zidane, mwenye umri wa miaka 43 kuwa mrithi wa viatu hivyo.



Uteuzi wa Zidane kuinoa Real Madrid unamfanya mwanasoka huyo wa zamani kuwa 
kocha wa 11 katika miaka 12 ya uongozi wa  Florentino Perez's.
Swali kubwa la kujiuliza je ujio wa Zidane kuinoa timu hii utazaa matunda au nae atafuatana na Bnitez, Ancelotti na The special One

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment